Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Inasimuliwa kuwa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, pamoja na mke wake Michelle Obama, waliwahi kualikwa katika mgahawa mmoja wa kifahari sana. Wengi walidhani mwaliko huo ulitokana na hadhi yao ya kisiasa, umaarufu au utajiri wao.
Lakini ukweli uliosimuliwa ni tofauti | Fuatilia maelezo haya na Sikiliza kwa Umakini Simulizi husika katika Klipu hiyo hapo juu.
Kwa ujumla, Wamiliki wa mgahawa huo walivutiwa zaidi na namna Barack Obama anavyomheshimu mke wake. Popote walipokuwa wakionekana pamoja, Barack Obama alikuwa akizungumza na Michelle kwa upole, akimsikiliza, akimheshimu mbele za watu, na kumthamini bila kujionesha au kujivuna.
Mmoja wa waliokuwa wakifuatilia mienendo yao alisema:
“Huyu ni mwanaume anayemheshimu mke wake kwa dhati, na heshima hiyo inaonekana wazi.”
Ndipo ikaeleweka kuwa mwaliko haukuwa kwa sababu ya cheo pekee, bali kwa sababu ya maadili.
Hapo ikathibitika kauli isemayo:
“Heshima huanzia nyumbani.”
Na pia:
Mwanaume anayemheshimu mke wake, huheshimiwa kila mahali.
Simulizi hili, kama anavyosisitiza Sheikh Abdallah Amani, linabeba funzo kubwa kwa jamii kwamba:
Heshima ya kweli haianzi mbele ya watu, bali huanzia ndani ya nyumba, katika namna mume na mke wanavyothaminiana.
Simulizi ya kweli kuhusu Barack Obama na Mke wake Michelle Obama -Msimulizi: Sheikh Abdallah Amani,akifikisha ujumbe wa maadili na Heshima katika ndoa
22 Desemba 2025 - 20:54
News ID: 1764974
Simulizi hili, kama anavyosisitiza Sheikh Abdallah Amani, linabeba funzo kubwa kwa jamii kwamba: Heshima ya kweli haianzi mbele ya watu, bali huanzia ndani ya nyumba, katika namna mume na mke wanavyothaminiana.
Your Comment